Tuesday, March 27, 2012

Count Down To Easter (Pasaka)


Wadau, 
Pasaka ndo hiyo around the corner…. Umeshapanga utaipa nini familia yako au wewe mwenyewe cha tofauti cha  kuongeza mvuto kwenye dining table yako ????  kwa ajili ya breakfast , au Easter Lunch or Dinner au zawadi kwa ndugu na jamaa
Sasa basi tumeamua kuwapatia aina mbalimbali za Cake nzuri za Pasaka na  jinsi ya kuziandaa, ili siku ya pasaka wote tuweze kufurahi na  fresh and delicious homemade cakes.

…. Lakini Kwanza si vibaya tukijua kidogo historia ya Pasaka na Tamaduni zake….


Yesu kristo alikufa msalabani siku ya ijumaa kuu zaidi ya  miaka 2000 iliyopita. Wakristu wanaamini  Yesu alifufuka  katika wafu siku ya jumapili. Siku Yesu alipokufa inaitwa ijumaa kuu na jumapili inayofuta ni  pasaka ( Easter ). Wakristo wanasheherekea ufufuko wa Yesu kila mwaka kati ya March 22 na april 25(The first Sunday after the vernal equinox)

Tamaduni za pasaka

Tamaduni za pasaka zinatofautiana kidogo duniani kote, lakini alama za pasaka ( Easter symbols ) ni sawa sehemu zote, hizo alama ni pamoja na  Easter Candles, Easter Cross, Easter Eggs, Easter Lamb, Easter lily, Easter Bunny, na Easter Hot cross Burns. Na Hapa chini  ni baadhi tu ya tamaduni hizo:

 Hot Cross Burns
Wakristu wanakuwa na furaha na shamsham nyingi wakati wa pasaka ambao una umuhimu sana kwenye imani yao.wanakuwa na tafrija kubwa  na kupika vyakula vingi. Hizi Hot Cross Burns ni alama maalum kwa ajili ya Pasaka.Ule urembo juu yake unakumbusha msalaba amboa Yesu alisurubishwa juu yake, kwa hiyo hii ni ya maana sana kwa wakristu. Na hizi ni tamu sana.

Easter Cakes

Utamaduni wa kutengeneza keki kwa ajili ya pasaka  ulianza na Ancient Anglo- saxon community( hii ni jamii ya watu wa kabila tatu za kijerumani ambao walivamia na kukaa kusini- mashariki mwa Uingereza kwenye karne ya Tano). Hawa  walikuwa wanaoka keki ndogo za ngano, zilizoitwa hot easter buns kwa ajili ya deity( miungu yao). Ilikuwa ni kwenye tamaduni zao wakati wa spring kwa ajili ya kuomba afya.
Wakati ukristo ulipokuja  kanisa lilibadilisha wheat cakes  na kuleta mikate mitamu iliyobarikiwa na hapo ndipo utamaduni wa keki ya Pasaka ulipoanza. keki za pasaka zina majina tofauti kulingana na sehemu ilipotengenezwa.

Easter lily


Ua la lily lina umbo la tarumbeta, na ni  jeupe. Watu wanasherekea uhalisia wa maisha kupitia kwake, na inasemekana mara ya kwanza kabisa liliota sehemu ambayo Jasho la Yesu lilidondoka. Ua hili linaleta maisha mapya wakati wa pasaka.

 Easter Eggs

Watoto wa marekani na Canada wanasema Easter Bunny au Sungura analeta mayai wakati wa pasaka.Germany and England wanasema  the hare brings them. The hare anaonekana kama Sungura lakini ni mkubwa na ana miguu masikio na miguu mirefu. Lakini Italy, Belgium and France, watoto wanasema mayai ya pasaka  yanaletwa na kengele za kanisani. Kengele za kanisani hazipigwi tangu ijumaa kuu hadi jumapili ya pasaka, kwasababu hii wanasema kengele zinaruka kwenda Roma, na zinapokuwa zinarudi kwao wakati wa pasaka, zinadondosha mayai yenye rangi kwa ajili ya watoto. Mayai ya pasaka yamekuwa alama ya ufufuo wa Yesu na kuzaliwa upya kwa binadamu. Watu wengi wanapeana zawadi za mayai wakati wa pasaka. Mayai ya pasaka yanaonesha uzazi na mavuno mengi, yanatakiwa kuleta maisha mapya na furaha kwenye maisha ya watu.Lakini kuna vyakula vingi zaidi ya mayai kufurahia wakati wa pasaka. Wengine  wanapika mikate yenye ladha kama cake, cookies in shape ya lamb. na Hot cross Burns.

Easter Candles
Mishumaa ya Pasaka inawashwa wakati wa Pasaka kusherekea kukufuka kwa Yesu Kristu.Wakati huu watu wanakuwa na furaha na wanashirikiana kuwasha mishumaa ya pasaka makanisani kuonesha maisha mapya kwa ujumla wake.




Easter Lamb


 Kondoo wa pasaka ni alama kubwa ya pasaka duniani kote, kondoo anamuonesha Yesu na bendela ya ushindi. Na katika nchi nyingi za Ulaya anakuwa ni kivutio kikubwa kwenye meza ya chakula.



Easter Bunny

Easter Bunny watu wengi wanahoji.bila easter bunny tunaweza kweli kusherekea pasaka? Easter bunny ingawa ni kiumbe wa kushangaza lakini anapendwa sana na watoto na watu wazima. Huwa kuna kuwa na manunuzi mengi na mipango mingi wakati wa pasaka lakini kila mtu anasubiri kwa hamu easter bunny aje  na kumletea bahati njema na furaha kwake. Pasaka ilianza kusheherekewa siku nyingi sana. Watoto wanavaa kama easter bunny na nyumba zinapambwa na easter bunny pia.wanatengeneza viota na kuviweka kwenye bustani zao na kusubiri mayai yaletwe na Easter bunny.wanaokota mayai hayo na wanacheza nayo kwa furaha. 
Basi kwa ufupi sana hiyo ni historia ya tamaduni za pasaka zilizoko duniani kwetu. Kuanzia kesho tutaanza kujifunza jinsi ya kutengeneza keki za pasaka za aina tofauti tofauti. Usikosee kupita.


...........Kila la heri na kwaresma njema...............






2 comments:

Anonymous said...

woow!

Anonymous said...

bomba sana!