Wadau,
Pasaka ndo hiyo around the corner…. Umeshapanga utaipa nini familia yako au wewe mwenyewe cha tofauti cha kuongeza mvuto kwenye dining table yako ???? kwa ajili ya breakfast , au Easter Lunch or Dinner au zawadi kwa ndugu na jamaa
Pasaka ndo hiyo around the corner…. Umeshapanga utaipa nini familia yako au wewe mwenyewe cha tofauti cha kuongeza mvuto kwenye dining table yako ???? kwa ajili ya breakfast , au Easter Lunch or Dinner au zawadi kwa ndugu na jamaa
Sasa basi tumeamua kuwapatia aina mbalimbali za Cake
nzuri za Pasaka na jinsi ya kuziandaa,
ili siku ya pasaka wote tuweze kufurahi na fresh and delicious homemade cakes.
…. Lakini Kwanza si vibaya tukijua kidogo historia
ya Pasaka na Tamaduni zake….
Yesu kristo alikufa msalabani siku
ya ijumaa kuu zaidi ya miaka 2000
iliyopita. Wakristu wanaamini Yesu
alifufuka katika wafu siku ya jumapili.
Siku Yesu alipokufa inaitwa ijumaa kuu na jumapili inayofuta ni pasaka ( Easter ). Wakristo wanasheherekea
ufufuko wa Yesu kila mwaka kati ya March 22 na april 25(The first Sunday after
the vernal equinox)
Tamaduni za pasaka
Tamaduni za pasaka zinatofautiana kidogo
duniani kote, lakini alama za pasaka ( Easter symbols ) ni sawa sehemu zote,
hizo alama ni pamoja na Easter Candles,
Easter Cross, Easter Eggs, Easter Lamb, Easter lily, Easter Bunny, na Easter Hot
cross Burns. Na Hapa chini ni baadhi tu
ya tamaduni hizo:
Hot Cross Burns
Hot Cross Burns
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEha3v2kqhXInsD_tuZVO82a58jd_Lz7TmL9v8PIlR4cN2cNqXTKZ2YiovWLA90zGFlZaKO8ytDq05QtT0Ei5IsbbwSBJ9Y13hL8hZUV24jDU5Yn8h83E19g4kLaupKrj9iRs8O6yVcNX9l-/s320/hot+cross+burns.bmp)
Easter
Cakes
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgltysRCwIlEXa1CtagSnZ04r4A_9ZPetiwAYuP8Amz-3zhyphenhyphenPN-2bwQIxL3K5gJWwz1tkkr-AB1sFe0vg6_-xIMAXB_d3zIfLYpQLJzwVRn9Ve2QTHUfP1Ci4y4dLbS2k1XCdIgHc4Y6ekD/s320/easter+eggs.bmp)
Wakati ukristo ulipokuja kanisa lilibadilisha wheat cakes na kuleta mikate mitamu iliyobarikiwa na hapo ndipo utamaduni wa keki ya Pasaka ulipoanza. keki za pasaka zina majina tofauti kulingana na sehemu ilipotengenezwa.
Easter lily
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgeoVqVSOs5VI6zQ62SFsTU6xi-yaOEeqxZ_7BqTD_iS8gwaivnzxSE76FwSHyjO-O7Et8edtDEBTSHQKrWCP2x_1suHn84WxJHpZU2nvjgePwmWBoJfkPC2bTpZMk8KsrUIUCo0dP7n_bJ/s320/easter+lilies.bmp)
Ua la lily lina umbo la tarumbeta, na ni jeupe. Watu wanasherekea uhalisia wa maisha kupitia kwake, na inasemekana mara ya kwanza kabisa liliota sehemu ambayo Jasho la Yesu lilidondoka. Ua hili linaleta maisha mapya wakati wa pasaka.
Easter Eggs
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj5Bk2Uc_WNDEAwoC7Y84jLfjmUBsMkY0_218JT0Belz5PDNjCVQKNZzvaUhFW3qfv8m6HXsf7DMBo6xTqRadC56LlDmzcQxu41bNY2cO2e_qGhrGPgfaUU5ehTCCH9HNWUyVA7zAFepvhy/s320/easter+eggs+kubwa.bmp)
Easter Candles
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbvV9109RVltkEyZg173Madez9i2cQftnSBioG7ce9JKjDKWMiRb8QmYZVaYWst66FmebI-GcPirwN0KT3ISH-pbE92cPZhJjNMc7FQxrM3WT_Ob1NQfNp1MhKJFSf5e-jFzO6Gnx1S1Am/s320/candles.bmp)
Easter Lamb
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWCXQRXZVeNULrJ7Tr90tuNpQqAGhaYfIDfGJCndtoIw6gpaSYeYzzJzst2nK_hQZPE28wt1JwqfmJm5c64_paaOqVa8v2K4dHfW97U5PawKK20-YLQUdRxdbns-XaZMvxfplin6kluS1k/s320/lamb.bmp)
Kondoo
wa pasaka ni alama kubwa ya pasaka duniani kote, kondoo anamuonesha Yesu na
bendela ya ushindi. Na katika nchi nyingi za Ulaya anakuwa ni kivutio kikubwa
kwenye meza ya chakula.
Easter Bunny
Easter Bunny watu wengi wanahoji.bila
easter bunny tunaweza kweli kusherekea pasaka? Easter bunny ingawa ni kiumbe wa
kushangaza lakini anapendwa sana na watoto na watu wazima. Huwa kuna kuwa na
manunuzi mengi na mipango mingi wakati wa pasaka lakini kila mtu anasubiri kwa
hamu easter bunny aje na kumletea bahati
njema na furaha kwake. Pasaka ilianza kusheherekewa siku nyingi sana. Watoto
wanavaa kama easter bunny na nyumba zinapambwa na easter bunny pia.wanatengeneza
viota na kuviweka kwenye bustani zao na kusubiri mayai yaletwe na Easter
bunny.wanaokota mayai hayo na wanacheza nayo kwa furaha.
Basi kwa ufupi sana hiyo ni historia
ya tamaduni za pasaka zilizoko duniani kwetu. Kuanzia kesho tutaanza kujifunza
jinsi ya kutengeneza keki za pasaka za aina tofauti tofauti. Usikosee kupita.
...........Kila la heri na kwaresma njema...............
2 comments:
woow!
bomba sana!
Post a Comment