Wednesday, March 28, 2012

Cupcake ya vanilla kwa ajili ya pasaka (Vanilla Easter cupcakes)


Ni rahisi kutengeneza, gharama ni ndogo na zaidi ya hayo ni tamu sana. 
·         Muda wa maandalizi: dk15
·         Muda wa mapishi : dk 25
·         Idadi ya keki: 12 
Mahitaji
  • Butter au Margarine yoyote gram 220
  • Sukari Gram 220
  • Mayai 2 makubwa
  • Unga wa ngano  gram 220, vizuri ukipata ule maalum kwa ajili ya keki
  • Vijiko viwili vya vanilla yogurt( huu ni mtindi ambao una ladha ya vanilla, unauzwa hasa kwenye supermarket, lakini kama ukiukosa unaweza tumia mtindi wa kawaida na vanilla ya kawaida)..
    Ni rahisi kutengeneza, gharama ni ndogo na zaidi ya hayo ni tamu sana. 

Kwa ajili ya kupamba  

  •  Unsalted Butter gram 80
  •     Icing sugar gram 250
  •     25g vanilla yogurt 
  •     Mayai madogo ya kupambia.( unaweza kuyatengeza kwa kutumia fondant za rangi mbalimbali, au ukanunua artificial, au ukachukua yai kabisa ukalichemsha na kulipaka rangi na kurembea keki yako. Mayai ndo yanaifanya keki hii iwe maalum kwa ajili ya pasaka) 

Jinsi ya Kuandaa

  1. Changanya butter na sukari pamoja, koroga hadi vilainike kabisa.Ongeza mayai kidogo kidogo huku unaendelea kukoroga. Kisha ongeza unga na maziwa koroga vizuri hadi vyote vichanganyike vizuri kabisa.Upate mchanganyiko ule mzito kiasi.
  2. Panga vikopo vya cupcake kwenye tray ya kuokea na uweke zile karatasi special ndani yake.
  3. Chota mchanganyiko wako na kijiko na kuweka kwenye hivyo vikopo kiasi cha nusu kopo.
  4. Oka hadi ziwe za brown ile brown nzuri kabisa ( golden Brown). Kisha ziache zipoe.
  5. Sasa tengeneza icing yako. Anza kwa kuchanganya butter na icing sugar, vipige hadi vichanganyike vizuri kabisa, na kama una ile mixer ya umeme ni nzuri zaidi kutumia. Weka mtindi na uendelee kuchanganya hadi iwe laini kabisa. Unavyochanganya kwa muda mrefu ndo inakuwa nyepesi zaidi.
  6. Kisha weka icing kwenye ile mashine ya kupambia keki au piping bag na utumie ile nozzle/mdomo yenye shape ya nyota. Anza kuweka icing kwa kuzunguka keki
  7. Lemba na yale mayai madogo.
  8. Unaweza ukaipamba na vitu vingine unavyopenda, kama chocolate, zabibu etc.




Keki hii ni tamu sana, familia itafurahia sana wakati wa pasaka

kama unahitaji  cake hizi wasiliana nasi kupitia tzcakes@yahoo.com au 0658-344 100 au 0718-733 318

No comments: