Mahitaji
·
150g
za unsalted butter
·
150g
Sukari
·
200g
unga wa ngano
·
Mayai
3
·
Chungwa
1 kubwa, maganda na juisi yake tu.
Kwa ajili
ya kupamba
·
Limao
1 kubwa, maganda na juisi yake tu.
·
Icing
sugar 175g
Jinsi ya kuandaa
1.
Changanya
Butter, sukari, na mayai, piga pamoja
hadi viwe laini kabisa. Ongeza unga na changanya tena vizuri.
2.
Weka
yale maganda ya machungwa na juisi ya machungwa kwenye huo mchanganyiko, kisha
koroga hadi vichanganyike vizuri.
3.
Weka
mchanganyiko wako kwenye chombo cha kuokea( na kumbuka kuweka mafuta kidogo
kwenye hicho chombo ili keki yako isishike chini). Sawazisha juu vizuri ili
upate level moja. Oka kwa dakika 30 au hadi uone keki yako imenyanyuka na
imekuwa na rangi ya dhahabu, na ukiishika inakuwa ngumu na imekaza, kama
unatumi jiko la umeme weka moto wa 180C au kama ni la mkaa ni kiasi ambacho
utaona kinafaa. Acha keki yako ipoe kwa dakika 5-10, kisha itoe na uiweke
kwenye sehemu nzuri, kavu na salama, wakati inasubiri kupambwa.
4.
Sasa
changanya icing sugar na maganda ya limao ( acha kidogo kwa ajili ya kupamba juu
ya keki) na juisi ya limao pamoja. piga hadi iwe laini na nyepesi kiasi. Kwa
kutumia kisu cha kupambia au chochote kitakacho faa, sambaza mchanganyiko huo
juu ya keki na acha udondoke pembeni mwa keki acha itulie vizuri. Sasa weka
yale maganga yaliyobaki na urembo mwingine wa pasaka hasa mayai( kama yale
tuliyojifunza hapo nyuma).
Hapa keki yako iko tayari kuliwa.
Inafaa kuliwa wakati wowote na watu wa rika zote. Unaweza kula na juisi, chai,
maziwa, soda au kahawa.
.......karibu sana.....
No comments:
Post a Comment