Habari zenu wadau wa tzcakes.....natumaini mu wazima wa afya tele....tukiwa tunaazimisha siku ya alhamisi kuu na kuelekea pasaka nakuletea aina nyingine ya cake ijulikanayo kama keki ya kikapu ya pasaka.....enjoy...
Keki hii ya kikapu ni keki haswa kwa
ajili ya pasaka. Ni rahisi na nzuri sana kwa wanaopenda kusheherekea pasaka.
Jinsi ya kuitengeneza ni hivi:
1. Tengeneza keki ya aina
unayopenda, chagua ladha na size unayopenda. Hii hapa ni keki ya 5-inch na
urefu wa 2.5 inches.
2. Kwa ajili ya kuremba tengeneza
icing recipe unayoipenda.( hapa tumetumia buttercream icing, ambayo ni icing
sugar,butter, maziwa na vanilla
3. Tengeneza shimo kidogo juu ya
keki( unatoa keki kidogo kwenye layer ya juu ya keki) au uanaweza kuzidisha icing pembeni mwa keki kama
unapenda icing. Sasa chukua machicha ya nazi, yanaweza kuwa yale special kwa
ajili ya kupambia keki au unawza tumia ya kawaida tu. Unaweza kuyakausha ua
kuyaacha vilevile. Yawekee rangi ya kijani na uyaweke hapo juu ya keki.
Sasa tengeneza mkono wa
kikapu.chukua foil na uikukunje iwe na U- shape na ifunike na ribbon au
karatasi yoyote nzuri. Sasa iweke kwenye keki yako.
Sasa kwenye lile shimo jaza pipi, Jelly beans,au pipi zozote
unazopenda.
Sasa keki yako iko tayari kwa kuliwa
Kuna keki za mbalimbali
za kikapu kwa ajili ya pasaka kama hizi;
Keki hii
ya chocolate, imerembwa na hiyo mistari ya kikapu imewekwa kwa kutumia uma,
unachora mistari iliyolala na iliyosimama.Ikawekewa machicha ya nazi kama
kawaida na juu yake ni Candy eggs......
Keki
nyingine ni hii utengenezaji ni uleule na upambaji ni ulelue. Hapa tu wameweka
machicha hadi pembeni mwa keki.
Unaweza kutengeneza hadi cupcakes za
kikapu!!!!
Umeona
aina mbalimbali za keki, hapa chaguo ni lako, unaweza kutengeneza keki ya aina
yoyote kwa ajili ya pasaka. Na ningependa unitumie picha ya keki yako
uliyotengeneza na hatua ulizofuata........
.......Nawatakia
Alhamis kuu njema......
No comments:
Post a Comment