Wadau,
Pasaka ndo hiyo around the corner…. Umeshapanga utaipa nini familia yako au wewe mwenyewe cha tofauti cha kuongeza mvuto kwenye dining table yako ???? kwa ajili ya breakfast , au Easter Lunch or Dinner au zawadi kwa ndugu na jamaa
Pasaka ndo hiyo around the corner…. Umeshapanga utaipa nini familia yako au wewe mwenyewe cha tofauti cha kuongeza mvuto kwenye dining table yako ???? kwa ajili ya breakfast , au Easter Lunch or Dinner au zawadi kwa ndugu na jamaa
Sasa basi tumeamua kuwapatia aina mbalimbali za Cake
nzuri za Pasaka na jinsi ya kuziandaa,
ili siku ya pasaka wote tuweze kufurahi na fresh and delicious homemade cakes.
…. Lakini Kwanza si vibaya tukijua kidogo historia
ya Pasaka na Tamaduni zake….
Yesu kristo alikufa msalabani siku
ya ijumaa kuu zaidi ya miaka 2000
iliyopita. Wakristu wanaamini Yesu
alifufuka katika wafu siku ya jumapili.
Siku Yesu alipokufa inaitwa ijumaa kuu na jumapili inayofuta ni pasaka ( Easter ). Wakristo wanasheherekea
ufufuko wa Yesu kila mwaka kati ya March 22 na april 25(The first Sunday after
the vernal equinox)
Tamaduni za pasaka
Tamaduni za pasaka zinatofautiana kidogo
duniani kote, lakini alama za pasaka ( Easter symbols ) ni sawa sehemu zote,
hizo alama ni pamoja na Easter Candles,
Easter Cross, Easter Eggs, Easter Lamb, Easter lily, Easter Bunny, na Easter Hot
cross Burns. Na Hapa chini ni baadhi tu
ya tamaduni hizo:
Hot Cross Burns
Hot Cross Burns
Wakristu wanakuwa na furaha na shamsham
nyingi wakati wa pasaka ambao una umuhimu sana kwenye imani yao.wanakuwa na
tafrija kubwa na kupika vyakula vingi.
Hizi Hot Cross Burns ni alama maalum kwa ajili ya Pasaka.Ule urembo juu yake
unakumbusha msalaba amboa Yesu alisurubishwa juu yake, kwa hiyo hii ni ya maana
sana kwa wakristu. Na hizi ni tamu sana.
Easter
Cakes
Utamaduni wa kutengeneza keki kwa ajili ya pasaka ulianza na Ancient Anglo- saxon community(
hii ni jamii ya watu wa kabila tatu za kijerumani ambao walivamia na kukaa
kusini- mashariki mwa Uingereza kwenye karne ya Tano). Hawa walikuwa wanaoka keki ndogo za ngano,
zilizoitwa hot easter buns kwa ajili ya deity( miungu yao). Ilikuwa ni kwenye
tamaduni zao wakati wa spring kwa ajili ya kuomba afya.
Wakati ukristo ulipokuja kanisa lilibadilisha wheat cakes na kuleta mikate mitamu iliyobarikiwa na hapo ndipo utamaduni wa keki ya Pasaka ulipoanza. keki za pasaka zina majina tofauti kulingana na sehemu ilipotengenezwa.
Wakati ukristo ulipokuja kanisa lilibadilisha wheat cakes na kuleta mikate mitamu iliyobarikiwa na hapo ndipo utamaduni wa keki ya Pasaka ulipoanza. keki za pasaka zina majina tofauti kulingana na sehemu ilipotengenezwa.
Easter lily
Ua la lily lina umbo la tarumbeta, na ni jeupe. Watu wanasherekea uhalisia wa maisha kupitia kwake, na inasemekana mara ya kwanza kabisa liliota sehemu ambayo Jasho la Yesu lilidondoka. Ua hili linaleta maisha mapya wakati wa pasaka.
Easter Eggs
Watoto wa marekani na Canada
wanasema Easter Bunny au Sungura analeta mayai wakati wa pasaka.Germany and
England wanasema the hare brings them.
The hare anaonekana kama Sungura lakini ni mkubwa na ana miguu masikio na miguu
mirefu. Lakini Italy, Belgium and France, watoto wanasema mayai ya pasaka yanaletwa na kengele za kanisani. Kengele za
kanisani hazipigwi tangu ijumaa kuu hadi jumapili ya pasaka, kwasababu hii
wanasema kengele zinaruka kwenda Roma, na zinapokuwa zinarudi kwao wakati wa
pasaka, zinadondosha mayai yenye rangi kwa ajili ya watoto. Mayai ya pasaka
yamekuwa alama ya ufufuo wa Yesu na kuzaliwa upya kwa binadamu. Watu wengi
wanapeana zawadi za mayai wakati wa pasaka.
Mayai ya pasaka yanaonesha uzazi na mavuno mengi, yanatakiwa kuleta maisha
mapya na furaha kwenye maisha ya watu.Lakini kuna vyakula vingi zaidi ya mayai
kufurahia wakati wa pasaka. Wengine
wanapika mikate yenye ladha kama cake, cookies in shape ya lamb. na Hot
cross Burns.
Easter Candles
Mishumaa
ya Pasaka inawashwa wakati wa Pasaka kusherekea kukufuka kwa Yesu Kristu.Wakati
huu watu wanakuwa na furaha na wanashirikiana kuwasha mishumaa ya pasaka
makanisani kuonesha maisha mapya kwa ujumla wake.
Easter Lamb
Kondoo
wa pasaka ni alama kubwa ya pasaka duniani kote, kondoo anamuonesha Yesu na
bendela ya ushindi. Na katika nchi nyingi za Ulaya anakuwa ni kivutio kikubwa
kwenye meza ya chakula.
Easter Bunny
Easter Bunny watu wengi wanahoji.bila
easter bunny tunaweza kweli kusherekea pasaka? Easter bunny ingawa ni kiumbe wa
kushangaza lakini anapendwa sana na watoto na watu wazima. Huwa kuna kuwa na
manunuzi mengi na mipango mingi wakati wa pasaka lakini kila mtu anasubiri kwa
hamu easter bunny aje na kumletea bahati
njema na furaha kwake. Pasaka ilianza kusheherekewa siku nyingi sana. Watoto
wanavaa kama easter bunny na nyumba zinapambwa na easter bunny pia.wanatengeneza
viota na kuviweka kwenye bustani zao na kusubiri mayai yaletwe na Easter
bunny.wanaokota mayai hayo na wanacheza nayo kwa furaha.
Basi kwa ufupi sana hiyo ni historia
ya tamaduni za pasaka zilizoko duniani kwetu. Kuanzia kesho tutaanza kujifunza
jinsi ya kutengeneza keki za pasaka za aina tofauti tofauti. Usikosee kupita.
...........Kila la heri na kwaresma njema...............
2 comments:
woow!
bomba sana!
Post a Comment